728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, October 05, 2015

    DISPLINE: SIMBA YAJA NA DAWA YA WATORO

    Uongozi wa Simba
    umeanzisha mfumo wa
    kuwakata mishahara
    wachezaji wote
    watakaoshindwa kufanya
    mazoezi pasipo sababu ya
    msingi wala kutoa taarifa
    sehemu husika, jambo
    ambalo linamaanisha
    inataka kila mmoja kili
    yake iwepo kwa ajili ya
    kuisaidia timu.

    Ni wazi kuwa Simba bado
    inajijenga baada ya
    kupotea kimataifa katika
    misimu mitatu mfululizo,
    hivyo inahitaji kuwa na
    wachezaji wenye ari ya
    ushindi kwa timu nzima na
    wenye nidhamu ya kufanya
    mazoezi.

    Mratibu wa klabu hiyo,
    Abass Suleiman ‘Gazza’,
    Ijumaa aliwaweka kikaoni
    nyota wote na kuwaeleza
    utaratibu huo na kuwataka
    kila mmoja anapokuwa na
    udhuru ni lazima atoe
    taarifa sehemu husika na
    kwamba siyo jukumu la
    kiongozi kumuuliza
    mchezaji kwa nini hajafika
    mazoezini, vinginevyo
    wasilaumiane mwisho wa
    mwezi wakikuta akaunti zao
    zinapungukiwa.

    "Nilitaka kuwaweka wazi,
    kila mchezaji atambue kuwa
    asipokuja mazoezini,
    hakuna tena kiongozi
    kuanza kumtafuta mchezaji
    kumuuliza sababu za
    kutofika, badala yake
    mchezaji ndiye atoe
    taarifa kama atakuwa na
    udhuru. 

    Tumepanga yeyote
    ambaye atakosa mazoezi
    pasipo taarifa sehemu
    husika, wajibu wangu ni
    kurekodi watoro na mwisho
    wa mwezi tusije kulaumiana
    akikuta amekatwa
    mshahara," alisema Ally
    bila kufafanua watakuwa
    wakikata asilimia ngapi
    kila mchezaji anapokosa
    mazoezi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DISPLINE: SIMBA YAJA NA DAWA YA WATORO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top