728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, October 05, 2015

    KUHUSU ADHABU ALIYOPEWA JUMA NYOSSO, MDHAMINI WA MBEYA CITY, NASSOR BINSLUM, AMETOA KAULI HII:

    Nassor Binslum• 

    Nimekua nikiulizwa maswali mengi juu ya sakata la Juma Nyosso kutoka kwa marafiki, wateja wangu na wadau wa soka kwa ujumla mbona tukiwa kama wadhamini wa Mbeya City kupitia moja ya bidhaa zetu Rb Battery tumekua kimya na hatujatoa tamko lolote mpaka sasa...???


    Tamko langu kwa niaba ya kampuni yetu ya Binslum Tyres Co Ltd ni hili hapa........Tunalaani tukio hilo kwa nguvu zetu zote kwa Captain wa Timu ambae ndie muwakilishi mkuu wa Club, wadhamini pamoja na wananchi wa Mbeya kwa ujumla kwa tukio hilo alilomfanyia Captain mwenzake wa Azam Fc John Bocco ambalo ni tukio linalochukiza na sio tu kuuchafua mchezo wa soka bali pia kutuchafua sisi wadhamini na washirika wenzetu pamoja na wananchi wa mkoa wa Mbeya.............Binafsi na kwa niaba ya kampuni yetu tunaunga mkono adhabu kali aliyopewa Nyosso...........Mwisho ningependa kumalizia kuwaomba Chama cha Soka (TFF) na hata waandishi wa habari wafanye weledi huu wa kureport unyama wa aina hii sambamba na adhabu kali kwa Vilabu na Wachezaji wote nchini wenye tabia hizi chafu kwani siamini kama Nyosso hizi tabia ameanza leo au jana bali ni tabia alizotokanazo kote alipopitia lkn hakuwahi kuadhibiwa huko nyuma wala kurepotiwa ktk magazeti mpaka sasa amekua mchezaji wa Mbeya City na pia siamini mwenye tabia hizi chafu ni Nyosso peke yake bali wako wengi ktk wachezaji wetu tena wengine wakichezea vilabu vikubwa vyenye mashabiki wengi nchini lkn hatujaona hata siku moja weledi huu uliotumika kumtia Nyosso hatiani ukitumika ktk usawa uleule kwa matukio ya aina ileile
    USTAARABU KWENYE SOKA INAWEZEKANA


    (CHANZO:CHAMPION)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUHUSU ADHABU ALIYOPEWA JUMA NYOSSO, MDHAMINI WA MBEYA CITY, NASSOR BINSLUM, AMETOA KAULI HII: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top