728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 01, 2015

    HAYA NDIYO MAMBO 10 YALIYOKWAMISHA USAJILI WA DE GEA KWENDA REAL MADRID



    1)Manchester United haikufungua milango yeyote ya mazungumzo ya Uhamisho wa David De Gea hadi Jana Asubuhi.
    2)Real Madrid, ingawa inajua ugumu wa kufanya Dili hizi Siku ya mwisho, ilikubali kuzungumza.
    3)Wakati Manchester United wanaingia kwenye mazungumzo hapo Jana walitoa sharti la kufikia makubaliano na Kipa wa Real Madrid Keylor Navas ili ajiunge nao Msimu huu na wakajulisha wanaongea na Wawakilishi wake.
    4)Real Madrid na Manchester United zilikubaliana haraka Uhamisho wa Wachezaji hao Wawili. Baada ya kuhakiki Mikataba yote na kuwa na nia ya kukamilisha kila kitu kwa wakati katika Mtandao wa FIFA wa Uhamisho, TMS [Transfer Matching System] ikiwa na pamoja na Usajili kwa LFP, Ligi ya Spain, Real Madrid ilituma tena Mikataba kwa Man United Saa 13:39, Saa za Spain.
    5)Manchester United wakatoa majibu yao kwenye Mikataba na kuituma Saa 21:43, Saa za Spain, yakiwemo mabadiliko kidogo ambayo yote tuliyakubali ili tuwahi TMS na LFP.
    6)Real Madrid, baada ya kupata Saini za David De Gea na Keylor Navas, tulituma Mikataba hiyo kwa Manchester United Saa 23:32, Saa za Spain, tukingoja Manchester United wakamilishe Mikataba.
    7)Manchester United walifikia makubaliano na Wawakilishi wa Keylor Navas Saa 23:53, Saa za Spain, na wakati huo ndio wakatuma kwa Wachezaji kusaini.
    8)Manchester United wakaingiza kwenye Mtandao wa TMS taarifa zote za De Gea, lakini si Keylor Navas, Saa 00:00, Saa za Spain, na kutuma kwa Real Madrid muda huo huo pamoja na Mikataba iliyosainiwa. Real Madrid ilipokea Makabrasha yote Saa 00:02, Saa za Spain, na kujaribu kuingia Mtandao wa TMS wakati huo huo na kukuta umefungwa.
    9)Ilipofika Saa 00:26, Saa za Spain, Mtandao wa TMS uliruhusu Real Madrid kuingia ili kujaza Taarifa za De Gea kwa vile Dirisha la Uhamisho la England linafungwa Leo. Real Madrid, wakitarajia kufikiriwa na LFP, walituma Mikataba kwa LFP kwa ajili ya Usajili licha ya kujua Dirisha la Uhamisho limeshafungwa.
    10)Ni hakika, Real Madrid ilifanya kila kitu kilicholazimu, kwa wakati wote, kuhakikisha Uhamisho huu wa Wawili unakamilika.www.sokaintanzania.com
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HAYA NDIYO MAMBO 10 YALIYOKWAMISHA USAJILI WA DE GEA KWENDA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top