728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 15, 2015

    UHURU SELEMANI ATOA MBINU YA KUFANIKIWA KUPATA TIMU NJE YA NCHI

    Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Uhuru Selemani amewataka Watanzania kuondokana na uoga wa kujaribu na kuondoa hofu ya kuonekana wamefeli.
    Uhuru ambaye sasa anakipiga katika timu ya Royal Eagle alikopelekwa mkopo akitokea Jomo Cosmos, zote za Afrika Kusini amesema uoga unawaumiza Watanzania wengi.

    Uhuru, amesema uoga ni tatizo.

    "Hofu ya wengi ni kufeli, tena wanajua baada ya kufeli magazeti yatawaandika sana kwamba hawakuwa na lolote au wameshindiwa.

    "Lakini si vibaya kujaribu tena na tena, huwezi kujua timu unayofanya majaribio kocha anahitaji nini. Tena kama unaenda waambie haya ni majaribio yangu ya nne.
    "Kwani hata timu ikiona umefanya majaribio mara nyingi wanajua unakubali, ni mtu unayetamaniwa na timu nyingi,” alisema.

    Uhuru aliyewahi kuzichezea Coastal Union, Mtibwa Sugar na Simba amesema anaendelea kupambana licha ya ushindani mkubwa kisoka nchini humo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UHURU SELEMANI ATOA MBINU YA KUFANIKIWA KUPATA TIMU NJE YA NCHI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top