728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 01, 2015

    SIMBA YAENDELEZA DOZI ZENJI YAWAGONGA MABAHARIA 4-0

    Simba imetoa mafunzo ya soka kwa tiku ya Black Sailor
    kwa kuichapa kwa mabao 4-0.

    Black Sailor ambayo imepanda Ligi Kuu Zanzibar msimu huu ilikiona cha moto, kwani hadi mapumziko Simba ilikuwa ba mabao mawili.

    Abdi Banda ndiye alianza kuifungia timu yake bao dakika ya nne tu baada ya kupokea pasi nzuri ya Dani Alves au Hassan Kessy na Kadabra Ibrahim Ajib akaongeza la pili katika dakika ya 23.

    Simba ilipata mabao yake mengine katika dakika dakika 80 na 90 wafungaji wakiwa ni Elius Maguli na Boniface Maganga.

    Wakati wote, Kocha Dylan Kerr alikuwa akisisitiza timu hiyo kucheza kwa kushambulia sana.

    Hii ni mechi ya pili ya kirafiki ya Simba mjini hapa, mechi ya kwanza ilishinda kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na mkongwe Mgosi na Hamis Kiiza.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA YAENDELEZA DOZI ZENJI YAWAGONGA MABAHARIA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top