728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 01, 2015

    MCHEZAJI AGONGWA JIWE MECHI YAVUNJWA

    Kama unadhani vitendo vya kihuni kama ugomvi,matusi na kadhalika ni huku kwetu tu hebu sikia hii iliyomkuta nyota wa klabu ya Legia Warsaw Ondrej Duda.

    Duda ambaye ni kati ya nyota wanaowindwa kwa udi na uvumba na klabu ya Inter Milan ya Italia juzi usiku katika michuano kufuzu ya ligi ndogo ya Ulaya "Europa Ligi" alionja joto ya jiwe baada ya kugongwa na jiwe kichwani wakati akiitumikia klabu yake ya Legia Warsal ya Poland iliyokuwa ikivaana na klabu ya FK Kukesi.

    Duda raia wa Slovakia alikutwa na tukio hilo baada ya klabu yake kuwa mbele kwa goli 2-1 kitendo kilochowauzi mashabiki wa Kukesi na kuamua kuanza kurusha vitu mbalimbali uwanjani ikiwemo jiwe lililompata barabara nyota huyo kichwani na kudondoka chini huku akivuja damu nyingi.

    Kufuatia kitendo hicho kisicho cha kiungwana mwamuzi alipuliza kipyenga na kuuvunja mtanange huo dakika ya 51.Kufuatia tukio hilo FK Kukesi huenda wakanyang'anywa pointi tatu na kulimwa faini kubwa.

    .




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MCHEZAJI AGONGWA JIWE MECHI YAVUNJWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top