728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 05, 2015

    NYOTA QPR AFELI VIPIMO VYA AFYA SUNDERLAND AKOSA SHAVU LA KUCHEZA TENA EPL

    Matarajio ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya QPR Leroy Fer kucheza kwa mara nyingine katika ligi kuu ya nchini England maarufu kama EPL yameyeyuka baada ya nyota huyo Muholanzi kufeli vipimo vya afya katika klabu ya Sunderland mchana wa leo.

    Fer,26 ambaye alikuwa akitarajiwa kujiunga na klabu ya Sunderland kwa mkopo wa msimu mmoja baada ya klabu yake ya QPR kushuka daraja msimu uliopita alifika makao makuu ya Sunderland mapema leo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya yake lakini baada ya zoezi hilo kukamilika iligundulika kuwa nyota huyo ana tatizo kwenye goti lake hivyo hataweza tena kujiunga na klabu hiyo inayojipanga upya baada ya kukwepa kushuka daraja.

    Taarifa zaidi zinadai Fer bado hajapona vizuri goti lake aliloumia mwezi Februari ya mwaka huu licha ya kurejea tena dimbani mwezi April.

    Hii ni mara ya pili kwa nyota huyo kufeli vipimo vya afya,mara ya kwanza ikiwa mwaka 2013 pale aliposhindwa kujiunga na klabu ya Everton akitokea FC Twente lakini alipata bahati baada ya klabu ya Norwich City kuamua kumsajili hivyo hivyo.

    Msimu uliopita Fer aliichezea QPR jumla ya michezo 29 na kufanikiwa kufunga magoli sita akishika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo ya London.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NYOTA QPR AFELI VIPIMO VYA AFYA SUNDERLAND AKOSA SHAVU LA KUCHEZA TENA EPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top