Mlinda mlango wa Manchester United Muargentina Sergio Romero,28 ameibuka na kupinga vikali uvumi ulioenea kuwa mke wake Eliana Guercio aliwahi kufanya ngono na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero.
Eliana akiwa katika pozi uwanjani |
Romero ambaye amejiunga hivi karibuni na Manchesster United akitokea Sampodoria ya Italia akiongea na televisheni ya taifa ya Argentina amepinga uvumi kuwa alikuwa na ugomvi mkubwa na Aguero baada ya kugundua kuwa nyota huyo wa Manchester City aliwahi kufanya safari moja akiwa na Guercio mwaka 2006.
Akimuongelea mke wake Romero amesema “Nina mke mzuri na familia nzuri.Siyo jambo zuri kusikia watu wanaongea jambo kama hili kuihusu familia yako."
Akiongea kumuhusu Aguero, 27 Romero amesema: “Tumekuwa na urafiki kwa kipindi cha miak 10 sas,hebu fikiria.Sikuwahi kuongea nae kuhusu hilo,lakini kwasasa ntaongea nae.
Eliana, 37, akipangua skendo hiyo amesema: “Siyo mkweli.Sijawahi kuwa na uhusiano wowote na Aguero.Inanikera kuhusishwa na Kun [Aguero].
“Hii ni zaidi ya miaka 10 sasa na kwa kipindi hicho chote nimekuwa nikilipinga jambo hilo.Aguero mwenyewe simjui.Alimaliza Eliana.
Eliana na Romero walioana mwaka 2008 baada ya kuwa wachumba kwa kipindi cha mwaka mmoja na sasa wana watoto wawili.
0 comments:
Post a Comment