Graeme
Souness amepinga mawazo ya mchambuzi mwenzake wa soka anayedai kwamba kitendo
cha John Terry kutolewa jana katika mechi dhidi ya Manchester City ni kumtaarifa
mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abromavic kuwa maisha ya soka ya nahodha huyo
yanaelekea ukingoni.
Kwa mara
ya kwanza nafasi ya Terry ilichukuliwa na Kurt Zouma baada ya dakika 45 tu.
Haijawahi
kutokea Kwa Terry kufanyiwa 'sub' katika mechi 177 chini ya kocha Jose
Mourinho.
Akizungumza
kwenye uchambuzi wa baada ya mechi wa Sky Sports, Souness, anaamini Terry
alitolewa kwasababu tu ya presha ya Mourinho.
"Nadhani
Terry alikuwa bora kuliko Gary Cahill, sikuona kama alicheza vibaya. John Terry
ni kiongozi". Alisema Souness.
"Nadhani
kocha anajaribu kumwambia kwa vitendo mmiliki wa timu kwamba anahitaji
wachezaji zaidi. Kama stori ni za kweli basi anapenda wachezaji wengi
(Mourinho). Nadhani alikuwa anasisitiza hoja hiyo kwa vitendo akimtoa
Terry".
Souness alikuwa
anabadilishana mawazo na mchambuzi mwenzake, Niall Quinn, ambaye alidai kwamba
kitendo hicho ni dalili ya soka la nyota huyo wa zamani wa England kumalizika.
Quinn,
mchezaji wa zamani wa Manchester City anaamini sasa Terry anakabiliwa na
changamoto ya kupigania namba yake katika kikosi cha kwanza.
"Tuliona
picha zake akiwa kwenye benchi baada ya sub, naamini yeye mwenyewe ameshaanza
kuwaza kwamba anakwenda kugombania namba kwenye timu".
"Sidhani
kama Terry atacheza wikiendi ijayo (dhidi ya West Brom). Naamini ana kazi kubwa
ya kumshawishi kocha wake. Huu unaweza kuwa mwanzo wa kuisha kwa soka
lake".
0 comments:
Post a Comment