Kikao
cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF )
kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini Cairo nchini Misri, kimewateua
watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbalimbali kwa kipindi cha
miaka miwili (2015-2017).
Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:
1.
Leodeger Tenga- (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati
ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za
Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya
Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama).
2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)
3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).
4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)
5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)
6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)
7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)
Shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote
walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la
kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
TFF.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment