Nusu saa baada ya kupokea kipigo cha bao 3-0 toka kwa Manchester City klabu ya Chelsea imetangaza kumsajili kwa mkataba wa miaka mitano mlinzi wa kushoto Mghana Abdul Baba Rahman toka klabu ya Ujerumani ya FC Augsburg kwa kitita cha €19.8m ambapo pamoja na bonasi kitita chicho kinaweza kuzidi €30m kiasi ambacho ni zaidi ya bajeti ya msimu mzima ya Augsburg.
Baba,21 anaiacha FC Augsburg baada ya kujiunga nayo msimu uliopita akitokea katika klabu daraja la pili ya Greuther Fuerth kwa ada ya €2.5m ambayo katika mauzo haya mapya itapokea asilimia 25 kama mkataba wa awali unavyosema.
Baba Rahiman ambaye pia aliwahi kuichezea klabu ya Asante Kotoko ya nyumbani kwao Ghana atakuwa akivaa jezi namba 17 Chelsea iliyowahi kuvaliwa na wakali kama Mohamed Salah,Scott Minto, Danny Granville, Albert Ferrer na Jose Bosingwa.
0 comments:
Post a Comment