Uongozi wa Simba umemtaka kipa mkongwe Ivo Mapunda kurejesha fedha alizopewa kwa ajili ya usajili wa mwaka mmoja.
Simba imeshindwa kumsajili Ivo ikidai hakuwa na ushirikiano na leo rasmi imetangaza kuachana naye.
Taarifa za ndani zinaeleza Ivo alilamba Sh milioni 8 kwa ajili ya usajili huo wa mwaka mmoja, lakini akaanza kuzingua kwenda kusajili.
Jitihada za kumpata ili asaini mkataba zilionekana kuwa ngumu huku akitoa visingizio kadhaa.
"Kweli Simba wameniambia natakiw akurudisha fedha, nakili nachukua fedha na nilikutana nao kwa ajili ya kusajili lakini wakasema hawatanisajili tena.
"Hakika nitarudisha, lakini nitahitaji muda hapo baadaye," alisema Ivo.
0 comments:
Post a Comment