728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 05, 2015

    AUDI CUP:BAYERN YAIGONGA AC MILAN 3-0,LEO KUIVAA MADRID KATIKA FAINALI

      Bayern Munich vs. AC Milan: Score and Reaction from 2015 Audi Cup Friendly
    WENYEJI Bayern Munich wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AC Milan jana katika mchezo wa Kombe la Audi Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.
     
    Kwa ushindi huo, Bayern Munich sasa itamenyana na Real Madrid katika fainali ya Kombe la Audi usiku wa leo, wakati AC Milan itawania nafasi ya tatu dhidi ya Tottenham iliyofungwa na Real 2-0.
     
    Mabao ya Bayern Munich jana yalifungwa na Juan Bernat dakika ya 24, Mario Gotze dakika ya 73 na Robert Lewandowski zikiwa zimesalia dakika sita. 
     lewa-milan
    Kiungo mpya, Arturo Vidal aliyesajiliwa kutoka Juventus ya Italia jana aliichezea kwa mara ya kwanza Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena. 
     
    Kikosi cha Bayern Munich kilikuwa; Ulreich, Rafinha, Boateng, Lahm/Alonso dk56, Kimmich/Alaba dk19, Hojbjerg, Rode, Bernat, Vidal, Costa/Lewandowski dk46 na Gotze.
    AC Milan; Lopez, De Sciglio, Zapata/Alex dk63, Ely, Antonelli, De Jong, Bertolacci, Bonaventura, Honda, Luiz Adriano na Bacca. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AUDI CUP:BAYERN YAIGONGA AC MILAN 3-0,LEO KUIVAA MADRID KATIKA FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top