728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 09, 2017

    Ronaldo,Zidane wachota tuzo Hispania


    Madrid,Hispania.

    STAA wa Real Madrid,Mreno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei wa ligi ya La Liga huku kocha wake Mfaransa ,Zinedine Zidane akishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi.

    Ronaldo,32 ameshinda tuzo hiyo baada ya kufunga mabao matano katika michezo minne iliyopita na kuisaidia Real Madrid kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa La Liga baada ya miaka mitano.

    Zidane yeye ametangazwa kocha bora wa mwezi baada ya Mei kuiongoza Real Madrid kushinda michezo yake yote na kuwapiku wapinzani wao Barcelona kwenye mbio za ubingwa wa La Liga.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ronaldo,Zidane wachota tuzo Hispania Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top