728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 09, 2017

    Bayern Munich kufanya kufuru ya mshahara kwa Alexis Sanchez


    Munich,Ujerumani.

    MIAMBA wa soka wa nchini Ujerumani,Bayern Munich wameripotiwa kuwa na mpango wa kumfanya staa wa Arsenal,Alexis Sanchez kuwa mchezaji anayelipwa pesa ndefu zaidi katika historia ya ligi ya Bundesliga ikiwa atakubali kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa Ujerumani.

    Taarifa kutoka nchini Ujerumani zinasema Bayern Munich wako tayari kumpa Sanchez,28, mshahara wa £350,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya ligi ya Bundesliga.

    Kwa sasa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Bundesliga ni mshambuliaji wa Poland,Robert Lewandowski anayelipwa £300,000 kwa wiki.

    Ikiwa usajili wa Sanchez utafanikiwa basi Lewandowski atakuwa ameondolewa kileleni mwa orodha ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi Bundesliga.

    Sanchez ameibuka kuwa chaguo la kwanza la wachezaji wanaohitajika Bayern Munich baada ya msimu huu miamba hiyo kuchesmsha kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.


    Ikumbukwe wiki iliyopita wakala wa Sanchez,Fernando Felicevich alisafiri mpaka Ujerumani kwenda kufanya mazungumzo na maofisa wa juu wa Bayern Munich kwa ajili ya kumtafutia changamoto mpya mteja wake.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bayern Munich kufanya kufuru ya mshahara kwa Alexis Sanchez Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top