Milan,Italia.
BAADA ya tetesi za muda mrefu hatimaye klabu ya AC Milan ya Italia imefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa VFL Wolfsburg ya Ujerumani,Mswisi Ricardo Rodriguez.
Rodriguez mwenye umri wa miaka 24 ameingia mkataba wa miaka minne na AC Milan mpaka Juni 2021 baada ya VFL Wolfsburg kukubali dau la €18m.
Rodriguez anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na AC Milan tangu ligi ya Seria A ilipomaliza michezo yake.Wengine ni Mateo Musacchio na Franck Kessié.
0 comments:
Post a Comment