728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 08, 2017

    HUYU HAPA:Man City yamnasa Éderson Santana de Moraes


    Manchester,England.

    BAADA ya kimya cha wiki moja hatimaye Manchester City leo imetangaza kumsajili mlinda mlango wa kimataifa wa Brazil,Éderson Santana de Moraes kutoka Benfica ya Ureno.

    Éderson mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Manchester City kwa mkataba wa miaka mitano baada ya Benfica kukubali ada ya £34.7 na kuwa mlinda mlango ghari zaidi duniani akiivunja rekodi ya Gigi Buffon aliyejiunga na Juventus mwaka 2001 akitikea Parma kwa ada ya £32.


    Ederson anakuwa mchezaji wa nne kutoka nchini Brazil kuwemo kwenye kikosi cha Manchester City.Wengine ni viungo Fernandinho na Fernando pamoja na mshambuliaji Gabriel Jesus.

    Ederson alianzia soka lake katika klabu ya São Paulo FC ambapo alidumu kwa miaka miwili kabla ya mwaka 2011 kujiunga na klabu ya daraja la pili ya Ureno ya Ribeirão.

    Akiwa na Ribeirão, Ederson alifanikiwa kucheza michezo 30 kabla ya msimu mmoja baadae kunyakuliwa na klabu ya ligi kuu ya Rio Ave aliyofanikiwa kuichezea michezo 63 katika kipindi cha miaka mitatu alichodumu na klabu hiyo.Mwaka 2015 alisajiliwa na Benfica ambapo alikuwa akitumika zaidi kwenye kikosi B kabla ya msimu uliopita kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha wakubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HUYU HAPA:Man City yamnasa Éderson Santana de Moraes Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top