728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 08, 2017

    PWAA:Yanga SC nayo yatupwa nje SportPesa Super Cup,saa fainali ni Wakenya tupu



    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    MABINGWA wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara,Yanga SC wameungana na vilabu vya Simba SC,Singida United na Jang'ombe Boys ya Zanzibar kutupwa nje ya michuano mipya ya SportPesa Super Cup baada ya kufungwa kwa penati 4-2 na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.

    Mchezo huo ulilazimika kutumia changamoto ya mikwaju ya penati kumpata mshindi baada ya dakika 90 kumalizika bila ya timu yoyote kupata bao.

    Yanga SC ambao katika michuano hiyo wameamua kutumia wachezaji chipukizi walishindwa kupeleka hatari yoyote ile langoni kwa AFC Leopards ambayo ilitinga nusu fainali ya kuitoa Singida United kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

    Penati za Yanga SC katika mchezo wa leo zimefungwa na nahodha Nadir Haroub Canavarro na Obrey Chirwa huku kinda Said Mussa Bakari na Said Juma Makapu wakikosa mikwaju yao ya penati iliyodakwa na kipa wa AFC Leopards,Otieno Ian.

    Penati za AFC Leopards zimefungwa na Bernard Mang'oli, Allan Kateregga Duncan Otieno na Ian Otieno .Marcellus Ingotsi alikosa mkwaju wake wa penati.

    Ushindi huo umeifanya AFC Leopards ifuzu fainali ambao itacheza na mshindi kati ya Nakuru All Stars na Gor Mania.Timu zote ni za kutoka Kenya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PWAA:Yanga SC nayo yatupwa nje SportPesa Super Cup,saa fainali ni Wakenya tupu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top