Paul Manjale,Dar Es Salaam.
NUSU FAINALI ya michuano mipya ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuchezwa leo kwa michezo miwili ya hatua hiyo kupigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza utakaochezwa saa 8:00 kamili mchana,mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara,Yanga SC watashuka dimbani kucheza na timu ngumu ya AFC Leopards kutoka Kenya.
Yanga SC ilifuzu nusu fainali baada ya kuwatupa nje miamba wa Kenya,Tusker FC kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kuisha kwa sare ya bila kufungana.AFC Leopards wao waliwatoa wageni wa ligi kuu bara,Singida United kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.
Nusu fainali ya pili itachezwa saa 10:00 jioni ambapo miamba wa Kenya,Gor Mahia na Nakuru All Stars watavaana kusaka timu moja itakayofuzu kucheza fainali na mshindi kati ya Yanga na AFC Leopards.
Mchezo wa fainali utachezwa Jumapili ya Juni 11ambapo mshindi atajishindia kitita cha Shilingi Milioni 60 za Kitanzania pamoja na kupata nafasi ya kucheza na miamba wa England,Everton ambao mwezi ujao watakuja nchini kucheza mchezo mmoja wa kirafiki.
0 comments:
Post a Comment