Lome,Togo.
BEKI wa Yanga,Vincent Bossou,amefunga bao moja na kuiwezesha timu yake ya taifa ya Togo kufuzu fainali za michuano ya AFCON baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Djibouti katika mchezo wa mwisho wa kundi A uliochezwa Jumapili usiku jijini Lome,Togo.
Mabao mengine ya Togo yametiwa kimiani na Mathieu Dossevi,Fo-Doh Laba na Komlan Agbegniadan aliyefunga mara mbili.
Matokeo hayo yameifanya Togo ifuzu ikiwa kama mshindwa bora (Best Loser) baada ya kushika nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 11 nyuma ya vinara wa kundi hilo la A Tunisia ambao wameichapa Liberia mabao 4-1 katika mchezo mwingine uliochezwa huko Tunis,Tunisia.
0 comments:
Post a Comment