728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 04, 2016

    KUFUZU KOMBE LA DUNIA: ENGLAND YAICHAPA 1-0 SLOVAKIA (+VIDEO)

    Malatinsky, Slovakia.

    Sam Allardyce 'Big Sam' amekianza vyema kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya England baada ya usiku huu kuiongoza miamba hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Slovakia katika mchezo mkali wa kundi F wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.

    Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Antony Malatinsky imeshuhudiwa bao la dakika ya 95 la kiungo Adam Lallana likiipa ushindi England dhidi ya Slovakia iliyokuwa imempoteza nahodha wake Martin Skrtel aliyelimwa kadi nyekundu dakika ya 54 baada ya kumkanyaga kwa maksudi mshambuliaji Harry Kane.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUFUZU KOMBE LA DUNIA: ENGLAND YAICHAPA 1-0 SLOVAKIA (+VIDEO) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top