Cairo,Misri.
HATIMAYE timu 16 zitakazoshiriki michuano ya kuwania ubingwa wa mataifa huru ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Gabon zimefahamika baada ya michezo ya mwisho kuchezwa jana Jumapili.
Ukiachana na wenyeji Gabon ambao wamefuzu moja kwa moja bila kumwaga jasho.Timu nyingine ambazo zimefuzu na kukamilisha idadi ya timu 16 ni:
Algeria,Burkina Faso , Cameroon,Cote d’Ivoire
DR Congo, Egypt, Ghana , Guinea Bissau , Mali ,Morocco,
Senegal , Togo , Tunisia, Uganda na Zimbabwe.
Uganda na Togo zimefuzu zikiwa kama washindwa bora (Best Losers) baada ya kumaliza katika nafasi za pili katika makundi A na D.
Uganda imemaliza ikiwa na alama 13,Togo imemaliza ikiwa na alama 11.Senegal imefuzu katika michuano hiyo ikiweka rekodi ya kuwa timu pekee iliyoshinda michezo yake yote sita ya hatua ya makundi.Guinea-Bissau imefuzu kwa mara ya kwanza.
Michuano ya AFCON itaanza kutimua vumbi lake Januari 14 nchini Gabon.
MATOKEO YOTE YA MICHEZO YA JUMAPILI
Malawi 1-0 Swaziland
Uganda 1-0 Comoros
Burkina Faso 2-1 Botswana
Zambia 1-1 Kenya
Congo 1-0 Guinea Bissau
Equatorial Guinea 4-0 South Sudan
Guinea 1-0 Zimbabwe
DR Congo 4-1 Central Africa
Mali 5-2 Benin
Niger 0-0 Burundi
Togo 5-0 Djibouti
Tunisia 4-1 Liberia
Morocco 2-0 Sao Tome
Algeria 6-0 Lesotho
0 comments:
Post a Comment