Wachezaji wa timu ya taifa ya El
Salvador wanasema kuwa wamekataa kuchukua hongo ili wakubali kushindwa
katika mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Canada siku ya
Jumanne.
Katika mkutano na vyombo vya habari,wachezaji wa timu
hiyo walicheza sauti ya mtu aliyejaribu kuwahonga kupitia kuwapatia
zawadi kadhaa.Canada ni sharti iishinde El Salvador huku
wakitumai kwamba Mexico itaishinda Honduras katika fainali ya mechi ya
kimakundi ili kuwa na fursa ya kuendelea.
El Salvador haiwezi kufuzu katika ya raundi ya mwisho ya kimakundi.
''Ni kisa kisicho cha kawaida kuweza kutokea'' ,alisema mwandishi mpekuzi wa BBC Declan Hill.
Zawadi kuu ambayo wangepata ni dola 3,000 kwa kila mchezaji.
Timu yote ilijitokeza na kocha wake na kusema kuwa walijaribiwa kuhongwa siku ya Jumamaosi.
Walicheza sauti ya dakika 11 ya mtu aliyejaribu kufanya uovu huo.Hill
anasema kuwa hongo hiyo ilidaiwa kutolewa na raia wa El Salvador ambaye
anawajua baadhi ya wachezaji,lakini ambaye alitaka kukisaidia kikosi
cha Honduras
0 comments:
Post a Comment