728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 06, 2016

    MKWASSA ATUPA KOMBORA CAF ADAI STARS INAPANGIWA MAKUNDI MAGUMU


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania,Charles Boniphase Mkwassa,amelitupia kombora shirikisho la soka Afrika (CAF) baada ya kudai kuwa limekuwa likiipangia timu hiyo makundi magumu katika michezo yake mbalimbali.

    Mkwassa ametupa kombora hilo leo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam baada ya kurejea nchini akitokea nchini Nigeria alikokwenda na Taifa Stars kuhitimisha michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON.  

    Mkwassa amesema kama Taifa Stars ingekuwa inapangwa katika makundi yenye timu za kawaida na mchekea kama Botswana ama Namibia basi ingekuwa inafika mbali na hata kufuzu michuano ya AFCON.

    Mkwassa ameitolea mfano timu ya taifa ya Uganda ambayo juzi Jumapili imefuzu michuano ya AFCON baada ya miaka 38 na kusisitiza kuwa Uganda imefuzu kwakuwa ilikuwa katika kundi jepesi tofauti na Stars ambayo kila mara imekuwa ikipangwa na timu vigogo Afrika kama Misri,Algeria na kujikuta ikiishia kufanya vibaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKWASSA ATUPA KOMBORA CAF ADAI STARS INAPANGIWA MAKUNDI MAGUMU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top