London, Uingereza.
BAADA ya kuanza msimu vizuri na kupata ushindi mfululizo hatimaye Chelsea imekwaa kisiki baada ya usiku huu kufungwa mabao 2-1 na Liverpool katika mchezo mkali wa ligi kuu Uingereza (EPL) uliochezwa katika uwanja wa Stamford Blidge.
Mabao yote ya Liverpool yametiwa kimiani kipindi cha kwanza na Dejan Lovren dakika ya 17 akiunganisha krosi ya Philippe Coutinho na Jordan Henderson dakika ya 36 kwa mkwaju wa mbali wa mita 30.
Bao la kufutia machozi kwa Chelsea limefungwa na Diego Costa katika dakika ya 59.Costa alifunga bao hilo akiunganisha krosi safi ya kiungo Nemanja Matic.
Matokeo hayo yameipandisha Liverpool mpaka nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu Uingereza sawa na Chelsea iliyo katika nafasi ya tatu.Timu zote zina alama tatu katika michezo minne.
Mwamuzi: Martin Atkinson
Watazamaji: 41,514
Vikosi
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, David Luiz,Azpilicueta, Kante, Willian (Moses 84′), Oscar (Pedro 84′), Matic (Fabregas 84′), Hazard,Costa.
Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Matip,Milner, Henderson, Wijnaldum (Stewart 89′),Lallana, Coutinho (Lucas 82′),Mane, Sturridge (Origi 57′).
0 comments:
Post a Comment