728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 16, 2016

    KLABU BINGWA AFRIKA:NUSU FAINALI YA KWANZA LEO NI ZAMALEK v WYDAD


    Alexandria,Misri.

    HATUA ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo kwa mchezo wa kwanza wa hatua hiyo kuchezwa huko Alexandria,ambapo miamba wa Misri,Zamalek watakuwa wenyeji wa Wydad Athletic Club ya Morocco katika uwanja wa Borg El Erab.

    SAFARI YA NUSU FAINALI ILIVYOKUWA

    Zamalek mabingwa mara tano wa michuano hiyo wamefika nusu fainali baada ya kuvitoa vilabu vya Union Douala ya Cameroon na MO Bejaia ya Algeria katika hatua za awali.

    Katika hatua ya makundi Zamalek walimaliza wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini waliyokuwa kileleni.

    Wydad,mabingwa mara moja wa michuano hiyo,wao wamefika nusu fainali baada ya kuvitoa vilabu vya AS Douanes ya Niger,CNaPS Sport ya Madagascar na TP Mazembe ya DR Congo.

    Katika hatua ya makundi Wydad walimaliza wakiwa katika nafasi ya kwanza mbele ya ZESCO United ya Zambia iliyomaliza katika nafasi ya pili.

    NUSU FAINALI YA PILI

    Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo itachezwa hapo kesho Jumamosi huko Johanesburg Afrika Kusini ambapo Mamelodi Sundowns watakuwa wakiikaribisha ZESCO United ya Zambia.

    Ikumbukwe bingwa wa michuano hii atajinyakulia zawadi ya kitita cha dola millioni 1.5 (Bilioni 2.7) pamoja na tiketi ya kuiwakilisha Afrika katika michuano ya klabu bingwa ya dunia itakayofanyika mwezi disemba nchini Japan.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KLABU BINGWA AFRIKA:NUSU FAINALI YA KWANZA LEO NI ZAMALEK v WYDAD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top