London,Uingereza.
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte,amefichua sababu inayofanya amweke benchi kiungo mahiri wa klabu hiyo Mhispania Cesc Fabregas na badala yake apendelee kumtumia zaidi kiungo Mbrazil Oscar Dos Santos.
Akifanya mahojiano kuelekea mchezo wa leo usiku wa ligi kuu dhidi ya Liverpool,Conte, amenukuliwa akisema kuwa udhaifu alionao kiungo huyo katika kukaba ndicho kitu pekee kinachomnyima nafasi ya kuwa katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kwasasa.
Conte ameongeza kuwa ameamua kumtumia zaidi Oscar badala ya Fabregas kutokana na kiungo huyo kuwa na uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja kitu ambacho Fabregas hakifanyi kwa usahihi unaotakiwa.Fabregas ni mzuri katika kushambulia pekee.
Wakati huohuo Conte amesema licha ya Fabregas kwasasa kuwa nje ya kikosi cha kwanza cha klabu hiyo lakini bado yuko katika mipango yake na katika mipango ya klabu hiyo.
Msimu huu Fabregas,27,amefanikiwa kucheza dakika 26 pekee katika michezo minne iliyopita ya ligi kuu England hali ambayo imeibua maswali mengi juu ya hatma ya kiungo huyo ndani ya klabu hiyo inayopambana kuhakikisha inaurejesha ubingwa wake iliyoupoteza msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment