728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 16, 2016

    MO AWEkA PESA MEZANI SIMBA IIUE AZAM


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameongeza ‘mzuka’ wa wachezaji baada ya kutoa ofa ya bonus ya Sh milioni 10 ili waweze kucheza kufa kupona na kuibuka na ushindi dhidi ya Azam.

    Simba wanatarajia kucheza na Azam kesho katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

    Mo ameahidi kutoa Sh milioni 10 ambayo itaongezwa na milioni 10 nyingine ambazo hutolewa na wanachama kwa kujichangisha na kufanya bonus ifike Sh milioni 20.Fedha hizo zitakabidhiwa kwa wachezaji ikiwa watashinda pambano hilo dhidi ya Azam.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, lengo la kufanya hivyo ni kuongeza morali ya ushindi kwenye pambano hilo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MO AWEkA PESA MEZANI SIMBA IIUE AZAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top