728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 09, 2016

    SIMBA SC YATOA ASANTE YA SIMBA DAY,YAWAKUMBUSHA YANGA KICHAPO CHA MEDEAMA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Uongozi wa klabu ya Simba na benchi la ufundi,kwa pamoja unawashukuru sana wanachama,washabiki wake na watu wote waliokuja jana kwenye sherehe za miaka themanini ya klabu yetu,ambazo zilijumuisha kilele cha wiki ya Simba Day ambazo zilifanyika jana tarehe 8-8-2016 katika uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam.

    Pia uongozi wa Simba unawashukuru sana kwa kwa ushangiliaji wenu wa 'NGUVU'uliochagiza ushindi mnono wa magoli manne kwa sifuri,dhidi ya timu kongwe kutoka Kenya AFC Leopards.

    Washabiki wetu mmeonyesha tofauti kubwa baina yao na sisi,kuujaza uwanja kiasi kile kwa viingilio vyenu wenyewe,na sio kuingizwa 'BURE' ilhali timu imetoka katika msimu ambao haukuwa na matokeo ya kuridhisha sana, ni ishara kuwa mna mapenzi makubwa sana na klabu yenu na uongozi unaamini hilo ni deni kubwa linalopaswa kulipwa kwa kuwapa furaha ktk msimu huu wa ligi 2016|17.

    Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha wale wanaotubeza, eti Leopards inashika nafasi za chini kwenye ligi kuu ya Kenya na ndio maana tukawafunga 4-0 wajiulize wao Medeama waliowapiga 'thalatha' walikuwa wanashika nafasi ya ngapi wakati wanawapa kile kisago cha mbwa mwizi? 

    Kimsingi timu mwalikwa kwenye tamasha la Simba Day lazima iwe inacheza ligi kuu ya kwao na iwe timu yenye historia ilioutukuka katika soka.

    AFC Leopards ni timu iliopo katika premier nchini Kenya na historia yake kwenye soka Afrika, huwezi kuilinganisha hata kidogo na Medeama ambayo iliwadhalilishaji 'WAKODISHWAJI'.

    Mwisho niwafahamishe kuwa timu yenu itaendelea na mazoezi kesho jumatano pale police kilwa road na weekend hii itaingia kambini,tayari kwa mchezo wa kwanza wa ligi kuu inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

    Imetolewa na HAJI S MANARA

    MKUU WA HABARI SIMBA SPORTS CLUB.(SIMBA NGUVU MOJ)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA SC YATOA ASANTE YA SIMBA DAY,YAWAKUMBUSHA YANGA KICHAPO CHA MEDEAMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top