728x90 AdSpace

Wednesday, August 17, 2016

OLIMPIKI:BRAZIL YATINGA FAINALI KWA KISHINDO YAIBOMOA HONDURAS 6-0,NEYMAR AFUNGA BAO LA MAPEMA ZAIDI

Rio de Janeiro,Brazil.

BRAZIL U23 imefanikiwa kufuzu fainali ya michuano ya soka la wanaume baada ya muda mfupi uliopita kuifumua Honduras U23 kwa jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa katika uwanja wa Estadio do Maracana uliopo Rio de Janeiro.

Neymar alianza kuifungua Brazil bao la kuongoza katika sekunde ya 15 ya kipindi cha kwanza na kuwa bao la mapema zaidi katika historia ya michuano hiyo kabla ya kufunga jingine dakika ya 90.


Mabao mengine ya Brazil yamefungwa na Gabriel Jesus aliyefunga mabao mawili dakika za 26 na 35 huku Marquinhos na Luan wakifunga bao moja kila mmoja dakika za 51 na 79.

Katika mchezo wa leo Brazil ilionekana kuwazidi karibu kila idara wapinzani wao Honduras na kuwafanya wacheze rafu za mara kwa mara.

Sasa Brazil inasubiri mchezo utakaochezwa baadae kati ya Nigeria na Ujerumani ili iweze kuijua timu itakayocheza nayo katika fainali siku ya Jumapili.

Vikosi

Brazil: Weverton; Zeca,Marquinhos, Caio, Santos; Walace,Augusto; Gabriel Barbosa, Luan,Gabriel Jesus; Neymar

Honduras: Lopez;Alvarez, Pereira, Palacios, Vargas,Garcia; Elis, Banegas, Acosta,Quioto; Lozano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: OLIMPIKI:BRAZIL YATINGA FAINALI KWA KISHINDO YAIBOMOA HONDURAS 6-0,NEYMAR AFUNGA BAO LA MAPEMA ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown