728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 20, 2016

    NIGERIA YATANGAZA 23 WA KUIVAA TAIFA STARS SEPTEMBA 3,OBI,IGHALO NDANI


    Lagos,Nigeria.

    KOCHA mkuu mpya wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) Mjerumani,Genort Rohr,leo Jumamosi ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini Agosti 28 mwaka huu kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kundi G wa michuano ya AFCON dhidi ya Taifa Stars.

    Kikosi hicho kitakuwa na Makipa watatu,Mabeki wanane,Viungo wanne na Washambuliaji wanane huku kikijumuisha pia mastaa wanaotesa katika ligi kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League (EPL).

    Mastaa hao ni pamoja na Mikel Obi, Ahmed Musa, Odion Ighalo,Victor Moses na Kelechi Iheanacho.Aidha katika kikosi hicho Rohr pia amewajumuisha wachezaji watano wanaoiwakilisha Nigeria katika michuano ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil.

    Wachezaji hao ni pamoja na Imoh Ezekiel, Emmanuel Daniel, Musa Muhammed,Abdullahi Shehu, Kingsley Madu pamoja na mshindi wa kombe la dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 17,Victor Osimhen anayeichezea klabu ya VFL Wolfsburg FC ya Ujerumani.

    KIKOSI KAMILI:

    Makipa: Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England); Emmanuel Daniel
    (Enugu Rangers); Ikechukwu Ezenwa (FC IfeanyiUbah)

    Mabeki: Leon Balogun (FSV Mainz 05,Germany); William Troost-Ekong (Haugesun FC, Norway); Chidozie Awaziem (FC Porto,Portugal); Jamiu Alimi (Kano Pillars);Abdullahi Shehu (Uniao da Madeira, Portugal);Musa Muhammed (Istanbul Basaksehir,Turkey); Elderson Echiejile (AS Monaco,France),Kingsley Madu (AS Trencin, Slovakia)

    Viungo: Mikel John Obi (Chelsea FC,England); Ogenyi Onazi (Trabzonspor, Turkey);Wilfred Ndidi (KRC Genk, Belgium); Nosa Igiebor (Maccabi Tel Aviv, Israel)

    Washambuliaji: Ahmed Musa (Leicester City,England); Kelechi Iheanacho (Manchester City,England); Moses Simon (KAA Gent, Belgium);Victor Moses (Chelsea FC,England); Imoh Ezekiel (Al-Arabi Sporting Club, Qatar), Odion Ighalo (Watford FC, England); Brown Ideye (Olympiacos FC, Greece); Victor Osimhen (Wolfsburg FC, Germany)

    Taifa Stars na Nigeria zitarudiana tena Septemba 3 mwaka huu huko Abuja.Mchezo huo utakuwa wa kukamilisha ratiba kwani tayari Misri imeshafuzu kutoka kundi hilo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NIGERIA YATANGAZA 23 WA KUIVAA TAIFA STARS SEPTEMBA 3,OBI,IGHALO NDANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top