London, England.
West Ham United imetangaza kuachana na mpango wa kutaka kumrudisha klabuni hapo Mshambuliaji wake wa zamani,Muargentina Carlos Tevez,baada ya staa huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester City na Juventus kutaka apewe mshahara £250,000 kwa wiki ili asaini kuichezea tena klabu hiyo aliyoinusuru kushuka daraja mwaka 2006-07.
Akitangaza uamuzi huo Mmiliki wa klabu hiyo, David Sullivan,amesema Westham United ilitaka kumsajili kwa mara nyingine Tevez,32,lakini kutokana na madai yake ya mshahara kuwa makubwa wameamua kuachana mpango huo.
Sullivan ameongeza kuwa uwezo wa klabu yake ulikuwa ni kulimpa Tevez mshahara wa £150,000 kwa wiki pamoja na bonasi nzuri ambayo ingemfanya awe mchezaji anayelipwa vizuri katika historia ya klabu hiyo.
Kwa sasa Tevez anaichezea klabu ya Boca Juniors ya nyumbani kwao Argentina baada ya kuachana na Juventus mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment