728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 04, 2016

    WATAKA NEYMAR ASHTAKIWE KWA UFISADI

    Brazil.

    Waendesha mashtaka nchini Brazil wamependekeza kwamba nyota wa timu ya
    Barcelona Neymar ashtakiwe na mashtaka matatu ya ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake hadi Barcelona.

    Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa ili kutumika kwa niaba yake ili mchezaji huyo
    alipe kodi ya kiwango cha chini.Maafisa nchini Brazil wanasema kuwa madai
    hayo dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia 2006.

    Madai hayo ni tofauti na
    yale ya kesi iliosikizwa siku ya Jumanne nchini Uhispania.Neymar alihudhuria kesi yake ya madai ya ufisadi kuhusu uhamisho wake.Amekana
    kufanya makosa yoyote.
    Waendesha mashtaka wa serikali ambao wanapendekeza kushtakiwa kwake wanadai kwamba kampuni zilibuniwa na fedha ambazo zingelipishwa kodi katika kiwango cha mtu
    binafsi zilitumwa katika kampuni hizo ili kupunguza ada hiyo.

    Ni mapema mno.Madai hayo ya viongozi wa mashtaka
    yatakwenda kwa jaji ambaye ataamua iwapo kuna kesi ya kujibu au la.kwa sasa Neymar
    sio mshtakiwa.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WATAKA NEYMAR ASHTAKIWE KWA UFISADI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top