Danny Welbeck juzi alirejea dimbani kukichezea kikosi cha vijana cha Arsenal kilipomenyana na kikosi cha vijana cha Brighton baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na majeruhi.
Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal wa London Colney Welbeck alicheza kwa dakika 60 kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Josh Dasilva. 
Welbeck hajaichezea Arsenal tangu mwezi Aprili mwaka jana baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo uliomalizika kwa Arsenal kwenda sare tasa dhidi ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment