728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 06, 2015

    LEWANDOWSKI AIUA MADRIA,BAYERN YATWAA AUDI CUP KWA MARA YA TATU


    Goli la mshambuliaji Robert Lewandowski limeipa ubingwa mwingine wa Audi Cup klabu ya Bayern Munich baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Real Madrid katika mchezo mkali uliopigwa usiku wa jana jumatano katika dimba la Allianz Arena mjini Munich.

    Lewandowski alifunga goli hilo dakika ya 88 baada ya kupokea pasi nzuri ya kinda Pierre-Emile Hojbjerg na kumfunga kirahisi kipa wa Real Keilor Navas.Kwa ushindi huo Bayern imefanikiwa kunyakuwa taji hilo kwa mara ya tatu sasa tangu lilipoanzishwa mwaka 2009.

    Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo....

    Real Madrid Starting XI: Navas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Kroos, Casemiro; Isco, Cheryshev, Vazquez; Jesé.
    Bayern Munich Starting XI: Neuer, Rafinha, Benatia, Boateng, Alaba, Alonso, Lahm, Costa, Götze, Vidal, Müller.

    Katika mchezo uliopigwa mapema magoli ya viungo Nacer Chadli na Tom Carrol yaliipa Tottenham ushindi wa goli 2-0 dhidi ya AC Milan na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu ya michuano hiyo ya Audi Cup.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LEWANDOWSKI AIUA MADRIA,BAYERN YATWAA AUDI CUP KWA MARA YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top