728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 14, 2017

    WAMEPIGWA:Mabingwa Cameroon wagongwa 4-0 na Colombia kuelekea kombe la mabara


    Getafe,Hispania.

    MABINGWA wa Afrika,Cameroon wameonyesha dalili kuwa huenda wasifanye vizuri sana kwenye michuano ya kombe la mabara itakayoanza siku tano zijazo baada ya Jumanne usiku kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Colombia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Coliseum Alfonso PĂ©rez huko Getafe-Hispania.

    Shujaa kwa upande wa Colombia alikuwa ni mlinzi Yerry Mina aliyefunga mabao mawili.Mabao mengine ya Colombia yamefungwa na James Rodriguez pamoja na Jose Heribreto Izquiredo.


    Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Cameroon ikimaliza na wachezaji kumi baada ya mlinzi wake Roberg Tambe kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mwanzoni kwa kipindi cha pili kwa mchezo mbaya.

    Cameroon itarejea tena dimbani siku tano zijazo kucheza mchezo wake wa kwanza wa kimashindano pale itakapocheza na mabingwa wa Amerika Kusini,Chile katika mchezo wa kwanza wa kombe la mabara litakalofanyika nchini Urusi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAMEPIGWA:Mabingwa Cameroon wagongwa 4-0 na Colombia kuelekea kombe la mabara Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top