728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 13, 2017

    Aliyemvunja mguu Luke Shaw atua AS Roma


    Roma,Italia.

    AS ROMA imefanya usajili wake wa kwanza wa majira ya joto kwa kumnasa beki wa kati wa PSV Eindhoven ya Uholanzi raia wa Mexico,Hector Moreno kwa ada ya uhamisho ya €5m.

    Moreno mwenye umri wa miaka 29 amejiunga na AS Roma kwa mkataba wa miaka minne utakaomalizika mwaka 2021.

    Msimu uliopita Moreno aliichezea PSV Eindhoven jumla ya michezo 32 akifunga mabao saba na kuwa beki aliyefunga mabao mengi zaidi ligi kui Uholanzi.



    Mwaka 2015 Moreno aligonga vichwa vya habari barani Ulaya baada ya kumchezea rafu mbaya beki wa kushoto wa Manchester United,Luke Shaw na kumvunja vibaya mguu wake wa kushoto kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Aliyemvunja mguu Luke Shaw atua AS Roma Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top