Liverpool,England.
MLINDA mlango kinda wa England,Jordan Pickford (Pichani) amejiunga na klabu ya Everton akitokea klabu iliyoshuka daraja ya Sunderland kwa ada ya uhamisho ya £30m.
Pickford mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kufuzu vipimo vyake vya afya Alhamisi jioni.
Usajili huo unamfanya Pickford kuwa mlinda mlango ghali zaidi kwa upande walinda mlango raia wa England.Pia unamfanya kuwa mlinda mlango wa tatu ghali zaidi dunia nyuma ya Ederson Moraes wa Manchester City aliyenunuliwa kwa £34.7m na Gianluigi Buffon wa Juventus aliyenunuliwa kwa £32.6m.
0 comments:
Post a Comment