728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 16, 2017

    USAJILI:Leceister City yamsajili Maguire

    Leceister,England.

    MABINGWA wa zamani wa ligi kuu ya soka nchini England,Leicester City wameuongezea ugumu ukuta wao kwa kumsajili mlinzi wa kati wa Uingereza Harry Maguire kutoka klabu iliyoshuka daraja ya Hull City.

    Maguire mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Leicester City baada ya Hull City kukubali ada ya uhamisho ya £17m.

    Licha ya Hull City kushuka daraja hivi karibuni lakini Maguire alikuwa ni kati ya wachezaji wachache walioonyesha kiwango safi cha usakataji soka ambapo mpaka pazia la ligi linafungwa alikuwa amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 36 hali iliyofanya vilabu vingi vianze kumtolea macho.

    Maguire alijiunga na Hull City Julai 2014 akitokea Sheffield United kwa ada ya uhamisho ya £2.5m na kufanikiwa kucheza michezo sita tu kabla ya Februari 2015 kujiunga na Wigan Athletic kwa mkopo wa mwaka mmoja.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Leceister City yamsajili Maguire Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top