728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 16, 2017

    USAJILI:Everton yamnasa nahodha wa Ajax

    Liverpool, England.

    USAJILI:MIAMBA wa soka wa jiji la Liverpool,Everton wameongeza sura mpya kwenye kikosi chao kwa kumsajili nahodha wa Ajax ya Uholanzi,Davy Klaassen kwa ada ya uhamisho ya £23.6m.

    Klaassen mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitano utakaofikia tamati Julai 30,2022.

    Klaassen anayecheza nafasi ya kiungo cha ushambuliaji ameiacha Ajax akiwa ameifungia mabao 49 katika michezo 163.

    Msimu uliopita Klaassen aliiongoza Ajax kutinga fainali ya michuano ya Europa Ligi ambapo ilichapwa mabao 2-0 na Manchester United katika mchezo wa fainali uliochezwa huko Stockholm, Sweden.

    Pia aliiongoza Ajax kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uholanzi maarufu kama Eredevisie.

    Mwaka 2016 Klaassen aligonga vichwa habari baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Uholanzi. Tuzo ambayo hapo awali iliwahi kutwaliwa na wakali kama Ruud Gullit, Marco van Basten,Dennis Bergkamp na kocha wa sasa wa Everton,Ronald Koeman.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Everton yamnasa nahodha wa Ajax Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top