Nantes,Ufaransa.
MENEJA wa zamani wa Leicester City,Muitaliano Claudio Ranieri ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa klabu ya Nantes ya nchini Ufaransa.
Ranieri mwenye umri wa miaka 65 amejiunga na Nantes kwa mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Mreno Sergio Conceica aliyejiunga na FC Porto.
Hii ni mara ya pili Ranieri anarejea kufundisha soka nchini Ufaransa.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012-2014 pale alipopewa kibarua cha kuifundisha Monaco.
Vilabu vingine vilivyowahi kufundishwa na Ranieri ni pamoja na Napoli, Fiorentina,Valencia, Atletico Madrid,Parma,Juventus,Roma na Inter Milan.
0 comments:
Post a Comment