London,England.
MABINGWA wa Kombe la chama cha soka nchini England FA,Arsenal wametangaza kumnasa mlinzi wa kushoto wa Bosnia, Sead Kolasinac.
Kolasinac mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Arsenal kwa mkataba wa miaka mitano akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani.
Mlinzi huyo anayetumia vyema mguu wa kushoto atakuwa akilipwa mshahara wa £130,000 na kuwa mmoja kati ya wachezaji wanapata mshahara mkubwa zaidi Arsenal.
0 comments:
Post a Comment