London, England.
MCHEZAJI bora wa mwaka wa Chelsea,Eden Hazard atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya jana Jumatatu kufanyiwa upasuaji kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia.
Hazard mwenye umri wa miaka 26 amelazimika kufanyiwa upasuaji huo baada ya juzi Jumapili kuvunjika mfupa wa ndani ya kifundo wakati akifanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Ubelgiji.
Hii ina maana kwamba Hazard atakosa michezo yote ya Chelsea ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu itakayofanyika katika nchi za China na Singapore.Pia Hazard anatarajiwa kukosa michezo ya mwanzo ya msimu mpya wa ligi kuu England pamoja na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Arsenal.
0 comments:
Post a Comment