Milan,Italia
MANCHESTER UNITED na Inter Milan zimekubaliana ada ya usajili ya winga wa kimataifa wa Croatia,Ivan Perisic.
Taarifa kutoka CalcioMercato zinasema Inter Milan imekubali kupokea ada ya £45m kutoka Manchester United baada ya awali kukataa ada ya £26m kwa ajili ya kumuuza winga huyo mwenye umri wa miaka 28.
Imeripotiwa kuwa tayari Perisic ameshakubali mkataba wa miaka minne wa kutua Old Trafford na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni £85,000 kwa wiki.
Vipimo pamoja na utambulisha vitafanyika wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment