Monaco,Ufaransa.
AS MONACO imeonyesha kuwa bado haina nia ya kuachana na staa wake Mfaransa,Kylian Mbappe hii ni baada ya leo kuripotiwa kuipiga chini ofa ya €100m (£87) iliyoletwa klabuni hapo kutoka Arsenal.
Kwa mujibu wa habari kutoka nchini Ufaransa,taarifa zinasema ofa ya Arsenal imekuwa ni ya tatu kupigwa chini na AS Monaco katika siku za hivi karibuni.
Mwishoni mwa mwezi uliopita AS Monaco iliripotiwa kukataa ada ya €120m (£105m) kutoka Real Madrid na kusisitiza kuwa nyota huyo mwenye miaka 18 ataendelea kubaki Stade Louis II.
Vilabu vingine vinavyodaiwa kuitaka saini ya Mbappe ni pamoja na Manchester United, Manchester City ,Chelsea, Bayern Munich na Paris Saint-Germain.
0 comments:
Post a Comment