728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 02, 2017

    Yanga: Simba inatibua usajili


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    BAADA ya Simba kufanikiwa kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani,gharama za kusajili wachezaji nyota zimeongezeka, imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.

    Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la FA wataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wakati mabingwa wa Ligi Kuu Yanga watapeperusha bendera ya nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema msimu huu watalazimika kuongeza bajeti kwa sababu wachezaji wamekuwa na nafasi zaidi ya moja katika kufanya uamuzi wa timu ya kujiunga nayo.

    Mkwasa alisema wakati Simba imekosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, gharama za usajili zilikuwa za kawaida, lakini msimu huu mambo yamebadilika.

    "Kiukweli uhitaji sasa umeongezeka, uhitaji umekuwa mkubwa, kila upande unahitaji kujiimarisha, kiasi cha fedha wanachotaka kimeongezeka na hii inatokana na kuwa na uhakika wa kucheza mashindano ya kimataifa," alisema Mkwasa.

    Alisema misimu miwili iliyopita klabu yake ilikuwa na uwezo wa kusajili kabla ya ligi haijamalizika, lakini msimu huu hilo halijawezekana.

    Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao waligoma kusaini mikataba mipya na sasa wako huru ni pamoja na Ngoma, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Ally Mustapha 'Barthezn na Simon Msuva.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga: Simba inatibua usajili Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top