Saint - Denis,Ufaransa.
OUSMANE Dembele (Kushoto) akishangilia bao baada ya kuifungia Ufaransa bao la ushindi katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya England katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Jumanne usiku kwenye uwanja wa Stade de France.
Mabao mawili ya mwanzo ya Ufaransa yalifungwa na walinzi Samuel Umtiti pamoja na Djibril Sidibe huku mabao yote ya England yakifungwa na nahodha wake Harry Kane.
Aidha katika mchezo huo Ufaransa waliokuwa wenyeji walilazimika kumaliza na wachezaji pungufu baada ya mlinzi wake wa kati Rafael Varane kutolewa nje kwa kadi ya nyekundu katika dakika ya 47 kwa kumwangusha ndani ya boksi Dele Alli.
0 comments:
Post a Comment