728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 09, 2017

    Hawa ndiyo walinda mlango 10 ghari zaidi duniani


    Manchester,England.

    JANA Alhamisi miamba wa soka nchini England,Manchester City walifanikiwa kukamilisha usajili wa mlinda mlango,Ederson Moraes kutoka Benfica ya Ureno.

    Usajili huo ambao umeripotiwa kuwa umeigharimu Manchester City kitita cha £34.85m mpaka kukamilika umemfanya Moraes anayetokea nchini Brazil kuwa ndiye mlinda mlango ghari zaidi duniani kwa sasa.

    Awali Muitaliano Gianluigi Buffon ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya kuwa mlinda mlango ghari zaidi duniani baada ya mwaka 2001 kujiunga na Juventus akitokea Parma kwa ada ya uhamisho ya £33m.

    Sasa Moraes yuko juu ya Buffon kwa tofauti ya £1.85m.Nafasi ya tatu inashikiliwa na Mjerumani Manuel Neuer ambaye mwaka 2011 aliihama Shalke 04 na kutua Bayern Munich kwa ada ya £19m.

    Wafuatao ni walinda mlango 10 ghari zaidi duniani

    1 Ederson £34.85m
    2 Gianluigi Buffon £33m
    3 Manuel Neuer £19m
    4 David de Gea £18m
    5 Claudio Bravo £15.4m
    6 Angelo Peruzzi £13m
    7 Jasper Cillessen £12.8m
    8 Jan Oblak £12.6m
    9 Petr Cech £10m
    10 Fraser Forster £10m


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hawa ndiyo walinda mlango 10 ghari zaidi duniani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top