728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 09, 2017

    Sitawaangusha mashabiki Azam FC


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MSHAMBULIAJI mpya wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Wazir Junior, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kuwa hatowaangusha.

    Junior aliyesaini mkataba wa miaka miwili amesema kuwa anafurahishwa kujiunga na Azam FC huku akidai zilikuwa ni ndoto zake za muda mrefu kutua kwa mabingwa hao.

    “Kwanza namshukuru mwenyezi Mungu kwa kujiunga na Azam FC, pili naishukuru timu yangu ya Toto African niliyocheza misimu miwili, nashukuru ushirikiano wa wachezaji wenzangu pamoja na viongozi na mashabiki,kingine nimefurahi kujiunga na Azam FC,” alisema.

    Alisema kuwa anaamini ya timu hiyo ndio mahali pake sahihi kwa kuendeleza kipaji chake huku akidai kuwa itamwezesha kufika mbali kwa kutimiza malengo yake ya kufika mbali yaani kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

    “Kwa hiyo nahitaji tu ushirikiano kwa mashabiki na wachezaji wenzangu,mashabiki wasiwe na wasiwasi waje kuisapoti timu yao uwanjani na nawahakikishia sitawaangusha,” alisema.

    Kwa upande wake, Jaffar, alisema kuwa wataendelea na zoezi hilo la usajili kwa kusajili wachezaji wengine kwa mujibu wa mapendekezo ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.

    “Kocha ameridhishwa na uwezo wa Wazir (Junior), uongozi ukapambana kuhakikisha unapata saini ya mchezaji huyo na hatimaye tumefanikiwa, ndio kwanza usajili tunauanza, lakini bado hizi ni kama mvua za lashalasha na masika yanakuja,” alisema.

    Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao saba msimu uliopita akiwa na Toto African, amekabidhiwa jezi nam asaba atakayokuwa akitumia msimu ujao, awali ilivaliwa na mshambuliaji aliyekuwa kwa mkopo Mtibwa Sugar,Kelvin Friday, kabla ya msimu uliopita Shaaban Idd kuitumia kwenye mechi za kimataifa za Kombe la Shirikisho Afrika (CC).


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Sitawaangusha mashabiki Azam FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top