Sousse,Tunisia.
TP MAZEMBE ya Congo DR imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika ( CAF Confederation Cup) baada ya Jumamosi Usiku ikiwa ugenini kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile Du Sahel katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali uliochezwa katika uwaja wa Stade Olympique de Sousse huko Sousse,Tunisia.
Wenyeji Etoile Du Sahel ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 20 ya mchezo kupitia kwa Lahmar Hamza.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili TP Mazembe waliwabana vizuri wenyeji wao Etoile Du Sahel na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 51 kupitia kwa Muivory Cost,Roger Assale na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Timu hizo zitarudiano tena Septemba 25 mwaka huko Lubumbashi,Congo,katika uwanja wa Stade TP Mazembe na mshindi katika mchezo huo atafuzu fainali ambapo atakwenda kupambana na mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Mo Bejaia ama FUS Raba
0 comments:
Post a Comment